KAULI YA ASASI ZINAZOFANYA KAZI NA WAFUGAJI WA ASILI KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI TANZANIA

UTANGULIZI:

Ufugaji wa asili

Ufugaji wa asili ni mfumo wa maisha unaohusisha matumizi ya ardhi ambapo wafugaji wanahama kwa mpangilio kutoka eneo moja hadi jingine kwa sababu maalum zikiwemo utafutaji wa malisho, maji na huduma zingine za mifugo baadaye kurudi kwenye maeneo ya awali kwa vipindi maalum.

Kutokana na hali halisi ya upatikanaji wa rasilimali za ufugaji asili nchini na kutofautiana kwa hali ya hewa kutoka eneo moja hadi jingine kwa kipindi cha mwaka, wafugaji wa asili hulazimika kuhama kutoka maeneo wanamoishi  na kwenda maeneo mengine na kisha kurejea katika maeneo ya awali kwa vipindi maalum.

Relevance: 
AttachmentSize
PDF icon Kauli ya wafugaji663.53 KB
Undefined