Mkutano wa hadhara wa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kusuluhisha migogoro ya Wafugaji na Wakulima Wilayani Mvomero

Kijiji cha Dihombo, 21 Februari 2016

Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, leo ameendelea kuongoza  viongozi wa Wizara, Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Mvomero katika kutatua mgogoro wa wafugaji na wakulima uliodumu tokea mwaka 1991. Mgogoro  huo wa wakulima na wafugaji unatokana na mwingiliano wa  maeneo ya malisho na kilimo umejenga uhasama, mapigano ya mara kwa mara ya  muda mrefu baina ya jamii hizo za wafugaji na wakulima.

Waziri alianza  harakati hizi baada ya wakulima  kukata mifugo ya mama  mjane Ketepoi tarehe 08 Februari 2016 ambapo Waziri alifika eneo la tukio na kufanya suluhu   tarehe 09 Februari 2016. Mkutano huu wa leo ambao ni wa pili wa Waziri huyo kushughulikia mgogoro huo, aliongozana na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi;  Wakurugenzi  wa Wizara; Mkuu wa Mkoa wa Morogoro pamoja na kamati ya ulinzi na uslama ya Mkoa; Mkuu wa wilaya ya Mvomero na kamati yake ya ulinzi na usalama ya wilaya; mkurugenzi wa Halamashauri ya wilaya ya Mvomero na timu ya wataalam wa halmashauri hiyo; Mbunge wa Mvomero, Madiwani na watendaji wa kata za Hembeti, Mkindo na Sungaji. Wakulima na wafugaji na viongozi wao wa vijiji waliohudhuria mkutano huo kutoka katika vijiji vya Hembeti, Bungoma, Dihombo, Mkindo na Kambala.

Waziri alisikiliza taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa kwanza kutoka ngazi zote za Mkoa, na Wilaya. Hatimaye aliwakutanisha viongozi wa  kata na vijiji, wakulima na wafugaji  kwa pamoja. Maazimio yafuatayo yalifikiwa:

  • Kuweka mpaka kuzunguka eneo lenye mgogoro  utakaotenganisha eneo la malisho  na kilimo. Hii itajumuisha kusafisha eneo  hilo lenye kilometer 11 kuzunguka  eneo lenye mgogoro yenye upana wa mita mita 7 kila upande ; na kuweka mfereji katikati ambao una kina cha mita  2 na upana wa mita 2.5. Waziri akawaasa wakulima na wafugaji wazingatie matumizi halisi ya neo hilo. Mkurugenzi wa halmashauri alitoa taarifa kuwa mkandarasi ameshapatikana toka kiwanda cha sukari Mtibwa na yupo tayari kunza kazi muda wowote kuanzia sasa
  • Kufanyika kwa mikutano ya maridhiano ya viongozi wa vijiji tarehe 09 March 2016, ukifuataiwa na mkutano wa  jamii ya wafugaji na wakulima kwa pamoja tarehe 10 Marchi 2016, na mwishoni mkutano wa majumuisho utakaohusisha watendaji, wakulima na wafugaji. Waziri kasisitiza Wizara  yake itawakilishwa kwa mapana katika kikao cha majumuisho
  • Kuimarisha mahusiano mema kati ya jamii za wafugaji na wakulima ili sheria ikichukuliwa itende haki. Hii  inajumuisha wakulima kufichua na kuwatolea taarifa wale  wenzao wanoharibu mali za wafugaji na wafugaji pia kuwafichua wenzao wanoharibu jina lao kwa wakulima
  •  Kamati za ulinzi na Usalama ziimarishe ulinzi na usalama kwa kadiri zinazvyowezekana kufika mbele ya tukio kwa wakati. Wizara itashirikiana na viongozi wa mkoa na wilaya kuhakikisha kuna bajeti ya kutosha kuwezesha kuimarisha ulinzi. Wafugaji na wakulima wasiharibu mfugo  hata mmoja, wala kulisha mazao katika  mashamba; akawaasa Wakulima na wafugaji kutoa  taarifa za uhalisia wa tukio kwa vyombo husika kabla mgogoro haujafikia katika hatua ya kuharibu mali na amani. Amesisitiza kuwa serikali ya wilaya na mkoa ikichelewa  kufika mbele ya tukio, wampigie simu, atafika yeye kwa wakati .
  • Serikali inaendelea kutafuta suluhisho la kudumu la mgogoro hii. Hii ni pamoja na wataalam wa Ardhi toka wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi tayari wameshafika mkoa Morogoro na wilaya ya Mvomero tayari kwa kuanza kazi na mwishoni mwa machi 2016, waziri wao takuja Mvomero kuhitimisha kazi. Pia waziri wa TAMISEMI anafika Morogoro kesho jumatatu na anategemea kufika wilaya ya Mvomero Jumanne kuendelea kutoa maelekezo sahihi kwa watendaji kumaliza kabisa migogoro hii.

Mbunge wa Mvomero aliwajulisha wananchi kuwa  wanaendelea  kumwomba Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuendelea  kurudisha mashamba mengine kwa wananchi.  Rais alirudisha mashamba 7 kati ya 33 yaliyopendekezwa kurudishwa kwa wananchi

Waziri pamoja na msafara wake alitembelea pia eneo linalotarajiwa kuwekwa mipaka, na akabainisha mapungufu machache ambapo wafugaji walidai hawakushirikishwa kwenye kuweka alama hizo hali iliyosababisha mpaka kuingia ndani kwa takribani kilometa mbili. Waziri amewaagiza  viongozi wa jadi wa wafugaji na wakulima wakae wafikie mufaka wa sehemu halisi   ambapo mpaka utapita kabla mkandarasi hajaanza kazi.

Waziri alihitimisha kwa kusema “Wote  tutabaki kuwa Watanzania, tusitofautiane kuendana na shughuli zetu za kiuchumi tunazofanya, wote tunategemeana kati yetu Wakulima na Wafugaji”. 

Mkuu wa Mkoa alimshukuru Waziri, alimhakikishia Waziri kuwa Serikali yake ya mkoa itatoa maelekezo kwa ngazi zote kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa, akasisitiza kuwa  hakuna aliye juu  ya sheria.  Na mwisho  ataendelea kuboresha ulinzi na usalama katika maeneo hayo. 

Relevance: 
Undefined