Mafunzo ya Stadi za Uongozi, Jinsia na Muundo wa Kitaasisi kwa Viongozi wa Wafugaji asili - Babati

Washiriki wapatao 27 kutoka katika vikundi na mitandao ya kiuchumi ya wafugaji wamepata mafunzo ya kuimarisha stadi za uongozi, jinsia na muundo. Katika ya washiriki 27, wanawake viongozi wa vikundi na mitandao ya kiuchumi ya wanawake walikuwa ni 16 kutoka katika vikundi vya Ombeni group – Meru, Baraza la Wanawake Monduli, Mtandao wa Wafugaji Kilindi, Chama Cha Wafugaji Babati, Kikundi Cha Mshikamano Cha Wanawake wa Lolela Gairo, Mtandao wa Wanawake Wafugaji Erreto Kiteto. Mafunzo yameandaliwa na TNRF program ya Wafugaji na kuendeshwa na Mkufunzi kutika shirika la undelezaji rasilimali watu la HACH kutoka Dar.

Mafunzo yamewajengea uwezo washiriki katika stadi za uongozi ambapo washiriki wameimarisha uwezo katika kutekeleza majukumu ya kiungozi na utawala ikiwa ni pamoja na kuandaa mipango ya vikundi/mitandao, kuratibu shughuli za vikundi, kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na kufanya tathmini. Pia wamejikumbusha sifa na wajibu wa kiongozi bora katika kufanikisha malengo ya pamoja ya vikundi/mitandao ya kiuchumi inavyokabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Washiriki walijadili na kubadilishana uzoefu katika kujenga mshikamano katika mitandao/vikundi vya kiuchumi vya wafugaji. Mafunzo yamewapatia mbinu na maarifa katika kuweka malengo ya pamoja na kuimarisha mshikamano miongoni mwa wanachama na viongozi.          

Mada ya kuandaa na kusimamia shughuli za mitandao/vikundi kwa kuzingatia kanuni na taratibu ilifundishwa kwa njia ya vibonzo, majadiliano na vikundi kazi. Mambo mbalimbali yameanishwa ikiwa ni pamoja kuimarisha uwajibikaji na uwazi kwa wanavikundi, kwa kuandaa taarifa na kuitisha vikao vya wanachama na kuzijadili. Washiriki wabaini jinsi kanuni na taratibu zinavywezesha kila mwanachama na viongozi pia kuzungatia misingi ya kikundi katika kufanikisha malengo ya kikundi.

Pia mafunzo yamewawezesha washiriki kuanisha vyanzo vya migogoro katika vikundi na namna ya kuitatua kwa kutumia mbinu shirikishi za kiutawala. Matumizi ya katiba za mitanda/vikundi na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuitisha mikutano ya wanachama yamefafanuliwa. Washiriki wamejifunza jinsi ya kutumia uongozi shirikishi katika kuepusha migogoro ndani ya vikundi.

Mafunzo yamewafungua washiriki na kuongeza ufahamu katika dhana na tafsiri za maneno yanayotumika katika kuelezea masuala yanayohusu jinsia na maendeleo. Tofauti kati ya jinsi na jinsia na mtizamo wa jamii kuhusu jinsia hasa katika jamii za kifugaji ulijadiliwa kwa kina. Wamejfunza mbinu za kuleta hamasa ya kijinsia katika familia, vikundi na jamii za kifugaji. Suala la mabadiliko ya tabia ya nchi na usawa wa kijinsia limefafanuliwa na kuwawezesha washiriki kutambua umuhimu wa wavulana, wanaume wasichana na wamawake kupata stadi za maisha zitakazowawezesha kutekeleza majukumu mbalimbali ya kijinsia kwa usawa.

Washiriki walipata nyenzo na mbinu za kufanya tathmini ya jinsia na kuibua ajenda muhimu katika jamii ambazo zitajadiliwa na wadau mbalimbali katika kuleta usawa wa jinsia. Washiriki wamechambua mgawanyo wa majukumu ya kijinsia katika ngazi ya familia na kubaini kuwa wanawake wanabebeshwa mzigo mkubwa na hivyo kuhitaji msaada wa wanaume. Pia masuala mbalimbali yanayohusu ubaguzi wa kijinsia katika familia na jamii katika masuala ya elimu na mgawanyo wa mali na umiliki wa rasilimali yameibuliwa. Washiriki wamejadili mambo mbalimbali yanayotakiwa katika kuleta usawa wa kijinsia na kuwa na mipango katika ngazi zote za familia, kijiji na jamii katika kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji maalum ya kijinsia.

Pia washiriki wamejifunza namna ya kuandaa na kusimamia kanuni na taratibu za mitandao/vikundi vya kifugaji vya kiuchumi. Vipengele muhimu vya kanuni za vikundi na mitandao ya kiuchumi vilianishwa, ikiwa ni pamoja na malengo, uanachama, shughuli kuu za vikundi, uongozi, ngazi za uongozi na maamuzi katika vikundi na mitandao, usimamizi wa rasilimali na fedha, namna na aina mbalimbli za usajili na hadhi za kisheria.

Washiriki wamepata wasaa wa kuandaa rasimu za kanuni na sheria (katiba) za vikundi na mitandao ya kiuchumi, katika ya vikundi 8 ambavyo viongozi wake wamepata mafunzo, vikundi 6 havikuwa na kanuni, vimewezseshwa na vimefanikiwa kuandaa rasimu ambazo wataziwasilisha na kuzijadili na wanachama katika vikundi na mitandao yao. Pia viongpai wa vikundi 2, wamepitia na kupendekeza maeneo ya kuboresha kanuni na taratibu za vikundi na mitandaoa yao.   

Category: 
Location: 
Babati - Manyara
Tanzania
TZ
When: 
18 May 2015 - 8:45am to 20 May 2015 - 6:45pm