SPIKA NDUGAI ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA

1.jpg

Media Folder: 

Jumuiko la Maliasili Tanzania kwa kushirikiana na wadau wake wamekutana na Spika wa Bunge la Tanzania pamona na zaidi ya Wabunge 90 Marafiki wa Mazingira “Tanzania Parliamentarians Friends of Environment (TAPAFE)”. Miongoni mwa wabunge hawa ni Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Maliasili na Utalii ambao nao walishiriki.

Lengo Kuu la mkutano huu ni kutathmini kazi za wadau zilizotekelezwa kwa kushirikiana na ofisi ya Spika wa Bunge pamoja na Wabunge wapenda Mazingira.

Kati ya mada zilizojadiliwa ni pamoja na mwingiliano wa sheria mbalimbali na jinsi zinavyoathiri utekelezaji wa majukumu kisekta. Ambapo katika hotuba yake Mh Spika amekiri kwamba kufikia malengo” “zipo sheria zenye matundu matundu ambazo zikiimarishwa zitaleta tija katika utekelezaji wake na hatimaye

Mh. Spika aliendelea kusisitiza kwamba: “Sote tu mashahidi wa mabadiliko ya Tabia Nchi na athari zitokanazo na mabadiliko hayo. Tunaona mvua nyingi zisizo za msimu na uharibivu mkubwa uliotokea kule Handeni na Korogwe na maeneo mengine…..

Mkutano huu na uzinduzi rasmi wa Mpango Mkakati wa TAPAFE ni ishara tosha na dhamira ya dhati ya ya Wabunge na mimi mwenyewe kama Mlezi wa TAPAFE katika kuonyesha juhudi za kutunza na kuhifadhi Mazingira yetu. Hivyo basi natambua na natoa wito wa kuendelea kushirikiana na Asasi za Kiraia kwenye utunzaji wa Mazingira.”

Mh Spika alitoa rai  kwa wabunge wote kwamba pamoja na agenda nyingine tunapokuwa tukizizungumzia kwenye utekelezaji wa kazi zetu agenda ya uhifadhi wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabia nchi  haiepukiki; tunahitaji mabadiliko ya kifikra ambayo ndio hasa yatakayoleta mageuzi kwenye suala zima la utunzaji na matumizi endelevu na Maliasili na Mazingira yetu.

Maazimio: Uongozi wa TAPAFE kufuatilia na kupata mrejesho kutoka kwa Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji kuhusu namna bora ya kuboresha mwingiliano wa sheria mbali mbali ikiwemo sheria ya Ardhi, Sheria ya Ardhi ya Vijiji, Sheria ya Wanyamapori, Sheria ya Madini, Sheria ya Mifugo na ile ya Nyanda za Malisho.

 

Relevance: 
Undefined